**********
Machifu nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuungana na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kuimarisha amani na Utulivu nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 22,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) aliyeambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi Mkoani Ruvuma alipokutana na Machifu kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini waliofanya ziara ya kutembelea Makumbusho ya Historia ya Vita vya MajiMaji Mjini Songea kama sehemu ya Maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuitembelea Makumbusho hiyo hapo kesho.
Mhe. Chana aliwahakikishia Machifu hao kuwa Wizara anayoingoza itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika Uhifadhi na kuendeleza urithi wa Kihistoria nchini ili watanzania waweze kunufaika na Mazao hayo ya Utalii wa Historia na Malikale.
Pamoja na kukutana na Machifu hao, Mhe. Balozi Chana amekagua maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Samia kwenye Makumbusho hiyo iliyohifadhi Historia adhimu na adimu katika ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla dhidi ya Ukoloni Miaka takribani 119 iliyopita.
Post a Comment