...................
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uagizaji Mchele nchini Comoro, Moussa Hamada na wamezungumzia namna bora ya kuongeza uagizaji wa bidhaa hiyo toka Tanzania.
Balozi Yakubu akimkaribisha Ubalozini hapo jijini Moroni alimueleza kuwa Tanzania yafaa iwe ndio chaguo la kwanza kuagiza bidhaa hiyo kwa kuzingatia ukaribu wa kijiografia, ubora wa mchele wa Tanzania, urahisi wa upatikanaji na pia idadi kubwa ya mavuno inayoongezeka kila mwaka nchini humo.
Balozi Yakubu alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa makongamano ya hivi karibuni yamebaini kuwa kuna uhitaji mkubwa na changamoto za kufanyiwa kazi baina ya Mamlaka yake yenye dhamana ya kuagiza mchele nje ya Comoro na wadau wa nje na kikao hicho kijadili namna bora ya kutatua changamoto tajwa.
Kwa upande, Bwana Moussa Hamada alimueleza Balozi Yakubu kuwa ni wakati muafaka kujadili kutokana na umuhimu wa bidhaa hiyo ambayo ndio chakula kikuu cha Comoro na kuarifu kuwa mahitaji ni takriban tani 300-350 kwa siku kwa visiwa vyote vinavyounda Comoro.
Balozi Yakubu alitumia fursa hiyo kumkaribisha afanye ziara nchini Tanzania ili kutembelea maeneo ya uzalishaji na kuonana na wadau muhimu.
Post a Comment