Tausi Mbowe
Banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), limekuwa kivutio kwa wananchi waliotembelea maonyesho ya Wiki ya Vijana Kanda ya Ziwa.
Maonyesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Furahisha vilivyopo Ilemela, jijini Mwanza pamoja na mambo mengine mamlaka hiyo imeendesha huduma za elimu kuhusiana na Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi.
Watumishi wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa leo Oktoba 10, 2024 pia wametoa huduma mbalimbali kwa wateja.
Miongoni mwa waliotembelea banda hilo ni pamonja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Jesca Lebba na wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani humo.




Post a Comment