CHALAMILA AWATAKA WANANCHI KULINDA AMANI NA KUIMARISHA MALEZI

 

*******


Timothy Marko

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wananchi wa wilaya ya Ilala na vitongoji vyake kulinda amani katika maeneo yao na kuimarisha malezi ya watoto na vijana.

Akizungumza jana katika ziara yake jijini Dar es Salaam, Albert Chalamila alisema hali ya kuongezeka kwa uhalifu katika wilaya hiyo inachangiwa na baadhi ya vijana kukosa malezi bora.

"Maeneo haya ya Pugu Stesheni, Gongolamboto kuna vibaka, lakini hali hii inachangiwa na malezi mabaya," alisema Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila.

Chalamila aliongeza kuwa, endapo watabaini mhalifu katika maeneo yao, wananchi wanapaswa kumpeleka kwenye serikali za mitaa ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Alisisitiza kuwa, tuhuma kwamba Rais amekuwa mtekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini siyo za kweli, na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo.

Aidha, Chalamila aliwasisitiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

"Ni vyema wakawachagua viongozi sahihi watakaowaletea maendeleo. Natoa ushauri kwenu, endeleeni kuwapima viongozi kwa sera na maendeleo," alibainisha Chalamila.

Chalamila aliwasisitiza wananchi kuwa ni vyema wakaendelea kufanya kazi kwa bidii, kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hawezi kuwaletea helak katika mifuko yao kama hawatafanya kazi kwa bidii.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ni wawote. Kama huna hela mfukoni, utakuwa na tatizo la akili," alisisitiza Chalamila.

Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi, amesema kuwa serikali inaendelea kuwapelekea wananchi wa Ukonga huduma za maji na barabara ili kuwaletea maendeleo. Alisema tayari serikali imeshatoa Shilingi bilioni 36 katika miradi ya maji katika bangulo kata ya Ukonga.












0/Post a Comment/Comments