EWURA YACHANGIA MADAWATI KWA WANAFUNZI 150 SHULE YA MSINGI KILOLENI


                       *********

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, leo, 11/10/24, imekabidhi madawati 50 yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi 150 wa shule ya msingi Kiloleni yenye usajili P1903011 iliyopo manispaa ya Tabora.

Mkuu wa Shule hiyo, Rajabu Kiama ameishukuru EWURA kwa kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule hiyo.

“Uongozi wa shule unatoa shukrani kwa EWURA kuunga mkono juhudi za kutatua changamoto hii ya upungufu wa madawati kwa wanafunzi, ambayo yatawapa fursa wanafunzi 150 kukalia madawati”, alisema

Ofisa Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Getrude Mbiling’i, akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Mamlaka, amewaasa wanafunzi wa shule hiyo kutunza samani walizopatiwa. 

Pia, alitumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme, gesi ya kupikia na utaratibu wa EWURA wa kushughulikia malalamiko yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa katika sekta za nishati na maji.

Kiloleni ni miongoni mwa shule kongwe iliyopo Kata ya Mapambano, Halmashauri ya Tabora na ilianzishwa mwaka 1970. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1050; wavulana 520 na wasichana 530 na jumla ya walimu 13.






0/Post a Comment/Comments