***********
Israel imethibitisha Jumatano kuwa ilimuua Hashem Safieddine, aliyetazamiwa kuwa mrithi wa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.
Taarifa hiyo imesema Safieddine aliuawa wiki
tatu zilizopita kufuatia shambulio katika vitongoji vya kusini mwa mji wa
Beirut.
Mkuu wa jeshi la Israel Luteni Jenerali Herzi
Halevi amesema kama walivyowafikia viongozi waandamizi wa Hezbollah, basi
watamfikia yeyote ambaye anatishia usalama wa raia wa Israel.
Hata hivyo kundi la Hezbollah halijathibitisha
taarifa hiyo.
Hayo yanajiri wakati Israel imeendeleza
mashambulizi yake huko Lebanon na katika Ukanda wa Gaza.
Umoja
wa Mataifa umelaani mauaji ya watu 18 kufuatia mashambulizi ya Israel karibu na
Hospitali ya Rafik Hariri mjini Beirut.
Jumuiya ya kimataifa imeendelea pia kutoa miito ya usitishwaji mapigano katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.
ccDWkiswahili
Post a Comment