*********
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James
Mataragio, amesema kuwa moja ya malengo ya Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi
(ARGeo-C10) linalofanyika nchini Tanzania ni kuwezesha Afrika kuongeza kasi ya
uendelezaji wa rasilimali ya Jotoardhi.
Amesema rasilimali ya Jotoardhi ikiendelezwa ipasavyo barani
Afrika itaweza kutumika kwa namna mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme pamoja na
matumizi mengine ya moja kwa moja kwenye Sekta ya Kilimo na Ufugaji.
Dkt. Mataragio amesema hayo jijini Dar es Salaam katika
hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Jotoardhi kwa washiriki wa Kongamano la
Kimataifa la ARGeo-C10 linaloendelea jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
programu za kongamano hilo.
“Tanzania ina maeneo mengi yaliyotambuliwa yenye viashiria
vya Jotoardhi na tayari Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TGDC) inaendelea
na shughuli za utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Songwe, Kiejo-Mbaka na
Ngozi.” Amesema Dkt.Mataragio
Ameeleza kuwa, kwa Tanzania kuweka mkazo kwenye uzalishaji
wa umeme kwa kutumia chanzo cha Jotoardhi kunaendana na malengo ya dunia ya
kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa ya ukaa kwani Jotoardhi ni
nishati safi.
Ametaja mafunzo yaliyotolewa katika Kongamano la Kimataifa
la ARGeo-C10 kuwa ni pamoja na uendelezaji wa mashapo ya Jotoardhi na
teknolojia mpya, Matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi katika sekta mbalimbali
ikiwemo kilimo na ufugaji hasa wa samaki pamoja na athari za masoko ya kaboni (carbon
markets).
“ Kwa kupitia mafunzo
haya tumezidi kujenga uwezo kwa vijana wa kitanzania ili kuweza kuendeleza
rasilimali ya Jotoardhi tuliyonayo kupitia Wataalam wabobezi katika
masuala yanayohusu nishati hii.” Amesema
Mataragio
Ametaja nchi mbalimbali zilizoshiriki mafunzo hayo
zinazojihusisha na rasilimali ya Jotoardhi kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda,
Ethiopia, Nigeria, Cameroon na New Zealand ambapo Tanzania imeweza kupata
uzoefu kutoka nchi nyingine zilizopiga hatua kubwa katika uendelezaji wa nishati
hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo, Bw.
Agnelli Kafuwe kutoka nchini Zambia, amesema kuwa yatasaidia katika kuisimamia sekta ya Jotoardhi kwani
wameongeza uelewa kuhusu nishati hiyo ikiwemo fursa na changamoto zinazoweza
kutokea katika usimamizi wake.
Amesema kuwa nishati ya Jotoardhi haihusishi umeme peke yake
hivyo lazima matumizi yake ya moja kwa moja yanayoweza kuboresha maisha ya watu
yapewe kipaumbele ikiwemo kupitia katika Sekta ya Kilimo.
Ametoa wito kwa nchi za Afrika kuunganisha nguvu ili kuweza
kupiga hatua zaidi katika uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi kama ilivyo
falsasa ya
Post a Comment