MAFANIKIO YA TEA CHINI YA DKT. KIPESHA: KUIMARISHA ELIMU TANZANIA KWA UZALENDO NA BIDII


1   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Mamlaka hiyo.

                                                              ***************

Bidii ya kazi na uzalendo ni nguzo muhimu zinazomwezesha mtu kufikia maendeleo binafsi na ya Taifa. Mfano mzuri ni China, ambayo imefanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa sababu ya uzalendo na juhudi za watu wake.

Ili kuimarisha utendaji wa kazi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda Taasisi mbalimbali na kuweka wasimamizi wa kuhakikisha maendeleo katika sekta kama elimu, ardhi, maji, umeme, na afya yanakua. Wakuu wa taasisi hizi wengi wao wanapatikana kutokana na elimu na uzoefu wao wa kazi.

Leo, napenda kumzungumzia Dkt. Erasmus Kipesha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ambaye anachukuliwa kama mzalendo akisimamia maboresho katika sekta ya elimu nchini.

 TEA, iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Na. 8 ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001, ina jukumu la kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Dkt. Kipesha na timu yake wamesimama imara kusaidia juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya elimu.

Dkt. Kipesha si mgeni ndani ya TEA; kwani alihudumu kama Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu. Ujuzi wake wa ndani umemuwezesha kuimarisha mikakati na kuchukua hatua za haraka katika kuinua ubora wa elimu na kuboresha miundombinu yake.

Katika kipindi hiki, tumeshuhudia maboresho makubwa ya miundombinu ya shule, ikiwemo madarasa, matundu ya vyoo na maabara za sayansi, hali iliyoongeza ufaulu wa wanafunzi. Kazi hii inahitaji kuungwa mkono na kila mtu anayeamini katika maendeleo, hasa katika sekta ya elimu, ambayo ni msingi wa maisha ya mwanadamu.

Dkt. Kipesha anaendeleza mawasiliano mazuri na watendaji wenzake, akichochea ufanisi wa miradi ya elimu. Shughuli kama maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu na Ujuzi zimeimarisha uwazi wa TEA kwa jamii.

Mafanikio haya yanathibitishwa na juhudi za TEA katika kutafuta rasilimali, ambapo kati ya mwaka 2019/2020 na 2022/2023, walikusanya Sh. 1.4 bilioni kutoka kwa wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania na TANAPA.

Katika moja ya kikao cha hivi karibuni na wasaidizi wake, Dkt. Kipesha alisisitiza umuhimu wa miradi ya TEA kuendana na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, ambayo inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Tunapaswa pia kutambua mchango wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Bi. Bahati Geuzye, ambaye alifanya kazi kubwa ndani ya TEA na sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Kupitia Serikali ya Awamu ya Tano, TEA imefanikiwa kufadhili miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Katika kuimarisha usimamizi, hivi karibuni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, ambaye ni mchapakazi na mbunifu. Tunaamini kuwa TEA itafanya vizuri zaidi chini ya uongozi wake.

Mafanikio haya yote yanafanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho ni Chama Tawala.

1.   Shule ya Serikali ya Mchepuo wa Kiingereza Msangalalee iliyojengwa na Mamlaka ya       Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa Jijini Dodoma.

1.                Muonekano wa ndani wa Shule ya Msingi Msangalalee iliyopo Jijini Dodoma.


2.                                        

1.  Muonekano wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Urughu Wilayani Iramba Mkoani Singida vilivyojengwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.

1.  Matundu 24 ya vyoo Shule ya Msingi Umwe iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani yaliyojengwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.

 Maabara ya Sayansi iliyojengwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa Shule ya Sekondari William Lukuvi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.

1.  Bweni lililojengwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa Shule ya Sekondari Mbomai iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

1.  Muonekano wa bweni lililojengwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa Shule ya Sekondari Mbomai iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

 


0/Post a Comment/Comments