........................
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Octoba 11, 2024 amewasili mji mdogo wa Ushirombo, Wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo atakuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Mwalimu Duniani kwa mwaka 2024.
Maadhimisho hayo yanafanyika leo kwenye Viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo ambapo pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Waziri Mkuu atakabidhi vifaa vya kujifunza na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi wilayani humo.
Majaliwa amepokelewa na Mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.
Post a Comment