********
Ili kusaidia wahanga wa ajali kupata huduma za uhakika katkka hospitali mbalimbali nchini ikiwemo ya kuongezewa damu Tamasha la magatu Tanxabua Automotive Festive (Autofest) limelenga kusaidia ukusanyaji damu.
Kwa kushirikiana na Damu Salama, wananchi watakaohudhuria tamasha hili la 12 kufanyika nchini watapata fursa ya kuchangia damu kwa ajili ya wahanga wa ajali mbalimbali za barabarani
Akizungumza na wanahabari Ally Nchahaga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments Ltd amesema Tamasha la mwaka huuli tafanyika katika viwanja vya Green Grounds (Farasi), Kinondoni huku Waziri wa Viwanda na Biashara akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.
‘’Tukio hili linahusisha moja ya maonyesho muhimu sana na yenye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto,” amesema.
Likirudi kwa mwaka wake wa Kumi na Mbili, tamasha la magari Tanzania Automotive Festival (Autofest) litakua likionyesha magari mapya, matoleo mapya, burudani za kusisimua kwa ajili ya familia nzima kuanzia Oktoba 26-27, 2024.
“Lengo letu ni kuendelea kuleta aina mbalimbali ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye ‘Autofest’ ili wadau wapate kujjfunza, kufurahia na kuridhishwa navyo,” amesema.
Mbali na maonyesho pia watu watapata fursa ya kupata elimu ya utunzaji sahihi wa magari kwani wengi wamekuwa wakishindwa kutokana na kukosa elimu hasa katika ulimwengu huu wa sasa ambao magari mengi yanatumia teknolojia sio sawa na yale ya zamani.
“Pia tukio hili la mwisho wa wiki linategemea kuvutia zaidi kwani mwaka huu tumeongeza kuchangiaji damu kushirikiana na DAMU SALAMA, kwani tunajua wahanga wa ajali wanavyotaabika juu ya mahitaji ya damu kutokana na upungufu katika akiba ya damu,” amesema.
Autofest ni tamasha maarufu la magari pekee Tanzania kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 imekua ni Tamasha muhimu katika masuala ya vyombo vya moto, likiwa ni onyesho pekee linalowaleta wapenzi wa magari pamoja.
Tamasha hili linabeba maonyesho ya magari ya abiria, magari ya biashara, pikipiki, michezo ya magari, na zana zinazohusiana na magari bila kusahau huduma shirikishi.
Burudani kwenye tukio zitahusisha, ‘Cone Challenge”; “Donuts” and “drifts” ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha ujuzi wakucheza na vyombo vya moto, Mafunzo ya kundesha 4x4 yakitolewa na Toyota Tanzania.
Pia kwa mujibu wa Nchahanga kutakuwa Ukaguzi wa magari bure kutoka kwa gereji mbali mbali, pia kutakuwa na ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani.
Tamasha hili litabebwa na kauli mbiu isemajo “Kuendesha kwa Kujihami ndio ufunguo wa Usalama Barabarani.
Tamasha hili linakwenda kufanyika pia ikiwa ni siku chache tangu Tanzania itoke kwenye maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani.
Post a Comment