MIONGOZO MINNE YA SAYANSI , TEKNOLOJIA NA UBUNIFU YAZINDULIWA

 WAKATI dunia ikiwa imejielekeza kwenye ubunifu wa Teknolojia na sayansi, serikali ya Tanzania imezindua miongozo minne inayochagiza maendeleo ya Sayansi, Ubunifu na Teknlojia.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 01, 2024 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carlyne Nombo  wakati wa  uzinduzi wa miongozo hiyo, uzinduzi uliofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Taifa ya Sayansi (Costech). Amesema  Costech imeanda muungozo hiyo ili kuwasaidia wabunifu wapite njia gani kufanikisha bunifu zao.

"Nchi nyingi zinaongozwa ubunifu unaofanywa na wananchi wao kupitia Costech serikali imetengeneza miongozo itakayokuwa inawasaidia hawa wabunifu kwenye kazi zao." Amesema Prof. Nombo

Prof. Nombo amesema kuwa miongozo hiyo itawawezesha watafiti kujipima juu ya tafiti zao,  kuna muongozo wa kupima vigezo vya kitafiti kujilinganisha na wenzetu ". 

Muongozo mwengine wa usambazaji wa takwimu watafiti wanapofanya tafiti zao wanatoa takwimu mbalimbali lakini huwezi kutoa takwimu bila kuwa muungozo tunasheria ya usambazaji wa taarifa hili linakusudia kulinda taarifa za watafiti wetu" Amesema Prof. Nombo


Kwa Upande wa  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi (Costech)  Dkt. Amos Nungu,  amesema kuwa watayapokea maelekezo yote kutoka kwa Serikali na watayafanyia kazi.

"Miongozo minne yote tutaisimamia kwa ukamilifu na kutoa mrejesho lengo ni kupata tija iliyokusudiwa, na miongozo hii imezinduliwa wakati muafaka" amesema Dk. Nungu.

Miongozo iliyozinduliwa leo na Bi. Nombo ni pamoja na Muongozo wa kitaifa wa kushirikiana kati ya Taasisi za Elimu ya Juu, Tafiti za Utafiti na Viwanda, Wa pili ni Muongozo wa Kitaifa wa upatikanaji hifadhi na usambazaji wa Takwimu za Sayansi na Teknolojia na ubunifu, Muongozo wa tatu ni Muongozo wa Taifa wa Uwezo wa Utafiti wa Kisayansi na Muongozo wa nne ni Muongozo Taifa wa Ubunifu.



















0/Post a Comment/Comments