************
Mwanadiplomasia kijana na mwanaharakati wa Mabadiliko ya
Tabianchi kutoka Tanzania, Sylviabay Kijangwa, amechaguliwa kuwa mjumbe wa
WiseYouth, chini ya Baraza la Wazee Afrika chini ya Baraza la Amani na Usalama
la Umoja wa Afrika akiiwakilisha kanda
ya Afrika Mashariki.
Sylviabay aliyechaguliwa Oktoba 01,2024 katika Makao Makuu
ya Umoja wa Afrika,Addis Ababa Ethiopia kwa kipindi cha miaka mitatu atachangia
katika kuzuia migogoro, upatanishi, na kushirikisha vijana katika juhudi za
kujenga amani barani Afrika.
Uteuzi huu unathibitisha nafasi yake muhimu kama
Mwanadiplomasia kijana mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya kijinsia,
mabadiliko ya tabianchi, migogoro na usalama, na kumuweka mstari wa mbele
katika kukuza uongozi wa vijana na amani endelevu barani Afrika.
Uteuzi huu unaonesha uzoefu wake mkubwa katika masuala ya
kijinsia, haki ya hali ya hewa, na amani, na unamtambulisha kama kijana
kiongozi anayesukuma mbele ajenda ya amani endelevu na uongozi wa vijana barani
Afrika.
Post a Comment