*********
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akishiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ametuma ujumbe wa wazi kwa vyama vya siasa kujipanga kikamilifu kwa uchaguzi huu badala ya kusubiria matokeo na kulalamika baadaye.
Hili linahusiana na ukweli kwamba vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, vimekuwa vikitumia muda mwingi kulalamikia mchakato wa uchaguzi kuliko kushawishi wananchi kuwaamini.
Badala ya kuzingatia kuwafikia wapiga kura na kueleza sera zao kwa kina, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vimejikita zaidi katika kuhoji uhalali wa mchakato wa uchaguzi na kutoa malalamiko mara kwa mara kuhusu mazingira ya uchaguzi.
Hii imewafanya kupoteza fursa ya kujiimarisha kama chaguo mbadala la kuaminika kwa wananchi.
Kwa wakati huu, badala ya malalamiko ya kila mara, upinzani unapaswa kuelekeza nguvu katika kuwashawishi wananchi na kujenga imani kwa wapiga kura juu ya uwezo wao wa kuongoza na kutatua changamoto zinazowakabili.
Ili demokrasia iwe na maana zaidi, vyama vya upinzani vinapaswa kujikita kwenye hoja za msingi na kujipanga vizuri katika kushindana kwa hoja, sera, na mikakati badala ya malalamiko yasiyokoma, ambayo yanaweza kuchosha wapiga kura na kuwatia shaka juu ya nia yao ya kweli katika kuleta mabadiliko.
Post a Comment