Meneja wa Program kutoka Shahidi wa Maji Pendo Hyera akizungumza kwenye warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imefanyika tar 9/10/2024 katika Hotel ya Morogoro mkoani Morogoro.

Afisa Tafiti kutoka Shirika la Shahidi wa Maji Mwajuma Salum akizungumza kwenye warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imefanyika tar 9/10/2024 katika Hotel ya Morogoro mkoani Morogoro.
Wadau wa maji kutoka katika Mkoa wa Dar es salaam wakijadili namna ya kupambana na uharibifu wa rasilimali za maji katika warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imefanyika tar 9/10/2024 katika Hotel ya Morogoro mkoani Morogoro.
Wadau wa maji kutoka katika Mkoa wa Morogoro wakijadili namna ya kupambana na uharibifu wa rasilimali za maji katika warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imefanyika tar 9/10/2024 katika Hotel ya Morogoro mkoani Morogoro.
Wadau wa Mashidi wa maji kwenye picha ya pamoja katika warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imefanyika tar 9/10/2024 katika Hotel ya Morogoro mkoani Morogoro.
........................
NA MUSSA KHALID,MOROGORO
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Shahidi wa Maji imeziomba Mamlaka zinazohusika na utatuzi wa changamoto za uharibifu wa vyanzo vya maji kuweka kipaumbele katika kufuatilia na kuzitatua kwa haraka ili kuepuka athari.
Hayo yameelezwa na Afisa Tafiti kutoka Shirika la Shahidi wa Maji Mwajuma Salum wakati akizungumza kwenye warsha maalum ya kuandaa mipango kazi ya kufuatilia changamoto za uwajibikaji wa maji katika jamii ambayo imewakutanisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo watendaji wa kata.
Mwajuma amesema Shirika hilo linahitaji ushirikiano kati ya wadau mbalimbali ikiwemo serikali kwa kuwa na daraja la mawasiliano ili jamii iweze kutapa nafasi ya kupeleka kero zinazoathiri maji na serikali iweze kutoa majibu kwa wakati.
Aidha ameisisitiza jamii kuhakikisha inatumia fursa hiyo kama jukwaa la kuangalia wanawezaji kuendesha dhana ya uwajibikaji kwa ujumla ili kuhakikisha vyano vya maji vinakuwa na usalama kwa Taifa.
“Pia malengo yetu sisi kama Mashahidi wa Maji ni kuhamasisha wananchi waweze kushiriki katika kusaidia serikali kuzitatua changamoto ambazo zinaharibu rasilimali maji”amesema Mwajuma
Awali akizungumza Meneja wa Program kutoka Shahidi wa Maji Pendo Hyera amesema kuwa wanaisaidi jamii waweze kuelewa wajibu na haki zao katika utatuzi wa changamoto ili kuwepo na uhakika wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Pendo ameeleza kuwa mkakati wao ni kuendelea kutoa ushirikiano kwa jamii na wadau mbalimbali kukaa pamoja na kujadili namna ya kupata suluhisho la vyanzo vya maji kuwa endelevu ili kusaidia vizazi vijavyo na vya sasa.
‘Licha ya kwamba wanajamii wamekuwa wakitumia vyombo vya habari na kupeleka malalamiko yao kwenye Mamlaka lakini zimekuwa hazipati majibu ya haraka hivyo tunaomba mamlaka husika kuweka kipaumbele katika kuzifuatilia na kuzipatia ufumbuzi kwani hali za vyombo vya maji zimezidi kuwa mbaya siku hadi siku”amesema Pendo
Kwa upande wao baadhi ya washirikiki akiwemo Afisa Mtendaji wa mtaa wa mfaranyaki Kata ya Tungi Mkoani Morogoro Veronika Luckas na Katibu wa Mtandao wa Maji Mkoa wa Dar es salaam Miraji Simba wamesema warsha hiyo imewaongezea ujuzi wa namna ya kufanya kazi ya kuzipambania rasilimaji za maji.
Wamesema kuwa watahakikisha wanaielimisha jamii kuepukana na kufanya uharibifu wa vyanzo vya maji ili kuepuna na changmoto zinazoweza kujitokeza kutokana na uharibifu huo.
Pia tutawaelimisha wanajamii kutoka fanya kilimo katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo ni kusababisha uharibifu na kuleta changamoto kwa watumiaji.
Imeelezwa kuwa kila mdau atakapowajibika katika kuvilinda vyanzo vya maji itasaidia kuongeza usalama kwa watu na taifa kwa ujumla.

Post a Comment