TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA KUSHIRIKIANA NA FINLAND KUTOA ELIMU JUMUISHI KWA WENYE ULEMAVU

 

*******

Na Timothy Marko

Ili kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika kupata elimu jumuishi, Taasisi ya Watu Elimu Wazima Wenye Ulemavu imeanzisha programu maalum ya kuwajengea uwezo watu hao ili waweze kupata elimu.

Akizungumza katika programu ya mafunzo ya elimu jumuishi kwa watu wenye ulemavu (MWAYODEO), Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Watu Wazima, Profesa Michael Ng'umbi, alisema kwamba taasisi hiyo imeanzisha mpango maalum wa kuwapatia elimu makundi maalum.

"TAASISI hii inalenga kufanya utafiti na kuwajengea uwezo makundi maalum katika elimu ya watu wazima," alisema Profesa Ng'umbi.

Profesa Ng'umbi aliongeza kuwa Diposa ni programu inayoweza kuwasaidia vijana na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake, Balozi Mdogo wa Finland nchini Tanzania, Tommio Lounio, alisema kuwa sensa ya mwaka 2022 ilionyesha kwamba asilimia 11.5 ya watu nchini ni walemavu, na ni muhimu kundi hilo kuweza kupata elimu. Alisema pia kwamba asilimia tatu ya watu wanaopata elimu ya watu wazima ni wenye ulemavu.

"Mradi huu unajumuisha kuwezesha miundombinu ya watu wenye ulemavu kupata elimu," aliongeza Balozi Mdogo wa Finland nchini Tanzania, Tommio Lounio.

0/Post a Comment/Comments