Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana
**********
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umetoa notisi kwa wadaiwa sugu 648 wa kodi ya pango ya sh. bilioni 14.8 katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha na Mara kwa lengo la kuanza kuwaondoa katika nyumba hizo.
Pia TBA imepata kibali cha Namba ya Makato Deduction Code (Vote No. S4 Code No.FC7801 TBA House Rent Contribution) kinachoruhusu mpangaji ambaye ni mtumishi wa umma kukatwa kodi katika mshahara wake na kumuepusha kulimbikiza madeni ya kodi ya pango.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kandoro alisema zoezi hilo la utoaji wa notsi limekuwa likitekelezwa chini ya Kampuni ya dalali wa Mahakama ya Twins Auction Mart ambapo wadaiwa hao tayari wamekabidhiwa notsi hizo.
Alisema zoezi hilo la utoaji notsi lilianza Septemba 17,mwaka huu, huku hatua ya kuwaondoa ikitarajiwa kuanza rasmi Jumatatu ya wiki ijayo.
"Zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu litaanza baada ya siku 14, kuanzia siku waliyopokea notisi za kulipa madeni yao ya kodi ya pango kukamilika na litaendelea nchi nzima kadiri ya notisi zitakavyoendelea kutolewa ,"alisema
Kandoro alisema TBA inadai jumla ya sh. Bilioni 14.884 huku fedha zinazodaiwa katika mikoa hiyo minne ya mwanzo ni Bilioni 1.764.
"Kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wapangaji wa nyumba hizi kutolipa kodi ya pango kwa wakati hali iliyosababisha kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi ya pango na kudhoofisha ukusanyaji wa mapato ya TBA,”alisema.
Alisema jambo la kulimbikiza madeni limekuwa kikwazo katika juhudi zao za kutekeleza mipango ya maendeleo kama vile kufanya ukarabati wa nyumba zilizopangishwa pamoja na kujenga nyumba mpya ambazo zitaweza kupangishwa au kuuzwa ukizingatia kuwa kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba bora za makazi.
Pia alisema TBA imeendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wapangaji wote wanaodaiwa ikiwemo kuwaondoa katika nyumba wadaiwa sugu kwa kutumia dalali wa Mahakama ambao ndio wamepewa zabuni hiyo kuwaondoa kwa niaba ya wakala.
"Jambo la kulimbikiza madeni limekuwa kikwazo katika juhudi za kutekeleza mipango ya maendeleo kama vile kufanya ukarabati wa nyumba zilizopangishwa pamoja na kujenga nyumba mpya ambazo zitaweza kupangishwa au kuuzwa ukizingatia kuwa kwa sasa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba bora za makazi,"alisema.
Alisema TBA imeendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wapangaji wote wanaodaiwa ikiwemo kuwaondoa kwenye nyumba kupitia dalali na hatua itakayofuata baada ya kuwaondoa katika nyumba hizo ni kuwafungulia kesi za madai kuhakikisha wanalipa madeni licha ya kuondolewa.
Hata hivyo alitoa wito kwa wapangaji wote zikiwemo taasisi za Umma, kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa wakati baada ya kupokea namba za kumbukumbu za malipo ambazo hutumwa kwao kila mwezi kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno.
Post a Comment