********
Kampuni ya Huduma za mawasiliano Nchini ya TIGO imeshinda Tuzo ya kimataifa ya Ookla (Speedtest Award 2024) ya Mtandao wenye Intaneti yenye kasi zaidi Nchini Tanzania ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika kipindi cha miaka miwili.
Tuzo za Speedtest Awards hutolewa na Taasisi ya Ookla iliyopo Seattle Washington Nchini Marekani ambayo inahusika na upimaji wa ubora wa Huduma na utendaji kazi wa mitandao mbalimbali ya simu duniani ambapo hutoa tuzo kwa mitandao inayofanya vizuri.
Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Tigo imeshinda Tuzo hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo ikitetea nafasi yake katika ubora wa kasi ya juu uliothibitishwa kimataifa wakati huu ambapo Kampuni hiyo inasherehekea miaka 30 toka kuanzishwa kwake Nchini Tanzania.
Post a Comment