****
Tausi Mbowe
Timu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imeibuka kidedea baada ya kushika nafasi ya pili katika mpira wa Pete.
TMDA iliibuka mshindi baada ya kuigaragaza timu ya Bohari ya Taifa ya Dawa (MSD), 44-21.
Awali TMDA iliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), 54 dhidi ya 47 kisha kuisambaratisha MSD.
Mashindano ya SHIMMUTA kwa upamde wa mpira wa Pete yamefkia tamati leo. November 25,
2024.
Maahindano hayo yanahusisha michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu, mpira wa Pete, kuruka, kuvuta kamba na kunyanyua vitu vizito.
SHIMMUTA ni mashindano yanayohusisha wafanyakazi kutoka serikalini na taasisi zake.
Post a Comment