TMDA YATOA POLE WALIOFUNIKWA NA GHOROFA KARIAKOO


 *****

Tausi Mbowe, Dar

Wakati Taifa likiendelea na maombolezo ya Vifo vya watu waliopoteza maisha baada ya ghorofa iliyopo Kariakoo kuporoka, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imetoa salam za pole. 

Ghorofa hiyo iliyokuwa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salam iliporomoka na kutitia Novemba 16,2024 na kusababisha vifo ladhaa na majeruhi.

Kupitia Bodi ya Ushauri kwa Wizara kwa TMDA (MAB), Menejimenti pamoja na watumishi wa Mamlala imetoa pole kwa Watanzania kufuatia tukio hilo. 

"Tunaungana na Watanzania wote katika kuomboleza vifo vya watu waliopoteza maisha baada ya ghorofa kuanguka" ilisema taarifa ya Mamlaka hiyo. 

Taarifa hiyo iliongeza kuwa,; " Mamlaka inatoa pole kwa wafiwa, majeruhi pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara wa Kariakoo kufuatia ajali hiyo. 

"Tuawaombea majeruhi wapone haraka na Mwenyezimungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina, "

0/Post a Comment/Comments