..............
Bei ya Korosho kwa msimu 2024/2025 imepanda mpaka kufikia Sh4,120 kwa kilo moja mkoani Mtwara.
Bei hiyo ambayo haijawahi patikana ukilinganisha na misimu mingine imepatikana baada ya kuzinduliwa kwa Mnada wa kwanza uliofanyika katika Wilaya ya Newala mkoani Mtwara unaoendeshwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Mnada huo umefanyika leo Ijumaaa, Oktoba 11,2024 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Newala umeshuhudia kilo moja ya Korosho ikuzwa kwa bei ya kati ya Tshs 4,120/= bei ya juu na 4,035/= bei ya chini.
Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumia Wilaya za Newala na Tandahimba (TANECU), kilipeleka sokoni jumla ya tani 3,857 za Korosho katika mnada huo, ambazo zote zimenunuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mnada huo, ameeleza kuwa huo ni mwanzo mzuri ambao unaonesha kuwa msimu wa Korosho 2024/2025 utakuwa wa manufaa kwa wakulima.
Kanali Sawala ameeleza kuwa zao la Korosho ni chanzo kikubwa cha uchumi katika Mkoa wa Mtwara, hivyo Serikali inayo furaha kuona kuwa bei zimechangamka na mkulima ataenda kunufaika.
Mkuu wa mkoa amewakumbusha wakulima kuzingatia ubora wa Korosho, hali ambayo itasaidia kuongeza thamani ya zao hilo katika minada inayofuata.
"Ubora huu unagusa kila eneo kuanzia kwenye kuvuna, kusafirisha, kuhifadhi maghalani nk. nitoe wito wa kila mmoja kwenye eneo lake
aendelee kusimamia ubora kulingana na maelekezo ya wataalam,na sisi ka.a tutaendelea kuwaunga mkono wadau katika kukuza sekta ya Korosho nchini" ameeleza
Msimu wa Korosho 2024/2025 umeanza wakati ambapo wakulima wana imani ya kuimarika kwa bei katika soko, huku uzalishaji ukitarajiwa kupanda kutokana na juhudi ambazo zimefanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kusimamia sekta ya Korosho nchini.
Post a Comment