Timothy Marko
TUME ya MADINI imesema imelenga kukusanya Shilingi trioni Moja kwa mwaka 2025 huku tume hiyo imesema Hadi kulifikia Mwezi October Mwaka huu Tayari imeshakusanya Shilingi bilioni 753.8 Kama Mapato ya Sekta hiyo.
Akizungumza naWaandishi wa Habari pamoja Wahariri wa vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendji wa Tume ya MADINI Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Tasisi hiyo mwaka 2018 tume ya MADINI imeweza kupata magari25 yanayokusanya Maduhuli ya SERIKALI.
"Tumeweza kudhibiti Hali ya utoroshwaji MADINI kwa kiasi kikubwa" Alisema Mhandisi Ramadhani Lwamo.
Lwamo Aliongeza kuwa Lengo la TAASISI hiyo nikuhakikisha Sekta ya MADINI ichangie Asilimia 10 ya Pato lataifa mwaka 2025 wakati Hadi kufikia 2023 Sekta hiyo imechangia Asilimia 7.2 ya Pato la taifa.
Alisisitiza kuwa katika mchango wa Ajira Nchini Sekta hiyo imezalisha Ajira kwa Asilimia 97.4 kwa wazawa wakati Ajira kwa Wageni ni Asilimia 2.
"Mikakati yetu katika Sekta ya MADINI ni kuimarisha udhibiti Biashara Haramu ya MADINI"Alibainisha Mhandisi Lwamo.
Post a Comment