Picha na Bbc
Wakati Watanzania wanajiandaa kwa
uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika Mwezi Novemba Mwaka huu, ambao
ni nyenzo muhimu kwa wananchi kushiriki kwenye mchakato wa maendeleo ya
kijamii, maswali makubwa yanaibuka kuhusu Chadema na viongozi wake.
Katika kipindi ambacho chama kinatakiwa kuwa mstari
wa mbele, mmoja wa viongozi wakuu, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, inasemeka hayupo
nchini na hajajisajili hata kupiga kura.
Tundu Lissu, akiwa Makamu Mwenyekiti
wa Chadema, ana wajibu wa kuwaunganisha wafuasi wake, kuwapa mwongozo, na
kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi.
Hata hivyo, kwa kushangaza, Lissu
amekaa nje ya nchi katika kipindi hiki muhimu.
Kutojisajili kwake kupiga kura
kunazua maswali juu ya dhamira yake na uaminifu wake kwa wafuasi wa Chadema na
Watanzania kwa ujumla.
Wafuasi wanahitaji kuona viongozi
wao wakiwa tayari na wenye dhamira ya kushiriki kikamilifu.
Pia, kutokuwepo kwa Lissu kunatuma
ujumbe ambao unaweza kuchukuliwa vibaya na wafuasi na kupunguza imani ya chama
mbele ya wananchi.
Hali hii inaweza kuashiria
changamoto ya uratibu na kujitoa kikamilifu ndani ya Chadema, ambayo ni muhimu
kwa chama chochote kinachotaka kuhamasisha ushiriki wa wapiga kura.
Inaonekana Chadema inakabiliwa na
changamoto ya kudhihirisha umoja na uongozi imara kwa wafuasi wao, hasa wakati
viongozi kama Lissu wanapokosekana kwenye kushiriki katika uchaguzi.
Ili Chadema iweze kuwa na athari
chanya na kuwa na uongozi unaoaminika, ni muhimu kwa viongozi wao kuwa mstari
wa mbele, kushiriki, na kuonyesha mfano kwa wananchi wanaowaongoza.
Kwa kuliona hili, Torchmedia tumemtafuta
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), John Mrema, kwa kumpigia simu ili kupata ufafanuzi juu ya
suala hili, lakini simu yake imekuwa ikiita pasipo kupokelewa.
Juhudi za kuwatafuta viongozi wa
chama hizo bado zinaendelea ili kufahamu juu ya suala hili. Endelea kufuatilia
torchmedia.co.tz.
Post a Comment