Ukarabati wa kisima cha gesi asilia unaoendelea katika Kitalu cha Songo Songo Mkoani Lindi unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kwa takribani futi za ujazo milioni 20 kwa siku.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika kitalu kicho Oktoba 26, 2024.
Mhandisi Sangweni alieleza kuwa kisima kinachofanyiwa ukarabati (SS7) kilipata changamoto ya kiufundi, hali iliyopelekea uzalishaji wa gesi asilia kutoka katika kisima hicho kusitishwa kwa muda.
Kwa mujibu wa maelezo ya Sangweni, ukarabati huo utagharimu takribani Dola za Marekani Milioni 20 na unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Novemba 2024.
“Ongezeko la futi za ujazo milioni 20 kwa siku unaotarajiwa mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wa kisima hiki unaweza kuzalisha mpaka megawati 100 za umeme” aliongeza Sangweni.
Uzalishaji wa gesi asilia kutoka katika Kitalu cha Songo Songo ulianza mwaka 2004 kwa lengo kuu la kuzalisha umeme.
Kwa sasa, Kitalu hicho kina jumla ya visima sita vinavyozalisha gesi asilia. Visima hivyo ni SS3, SS5, SS9, SS10, SS11 na SS12.
Kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024/25, uzalishaji wa gesi asilia kutoka katika Kitalu cha Songo Songo ulikuwa wa wastani wa futi za ujazo milioni 86 kwa siku.
Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mha. Charles Sangweni (mwenye fulana nyeusi) wakati wa ziara maalum katika Kitalu cha Songo Songo Mkoani Lindi ambapo kazi ya ukarabati wa kisima cha uzalishaji wa gesi asilia inaendelea. Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 26, 2024.Muonekano wa kisima namba 7 ambacho kinafanyiwa ukarabati katika Kitalu cha Songo Songo. Ukarabati huo utawezesha ongezeko la uzalishaji wa gesi asilia kwa takriban futi za ujazo milioni 20 kwa siku.Mkurugenzi Mkuu wa PUR Mha. Charles Sangweni (mwenye fulana nyeusi) na timu ya wataalamu wakiangalia kazi inayoendelea ya ukarabati wa kisima namba 7 cha uzalishaji wa gesi asilia katika Kitalu cha Songo Songo.Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mha. Charles Sangweni (mwenye fulana nyeusi) katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu mara baada ya kutembelea kisima namba saba cha uzalishaji wa gesi asilia kinachofanyiwa ukarabati katika Kitalu cha Songo Songo Mkoani Lindi.Mtaalamu kutoka kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ltd (mwenye nguo za light blue) akutoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa PURA (mwenye fulana nyeusi) na wataalamu kutoka PURA wakati wa ziara maalum katika Kitalu cha Songo Songo ambapi kazi ya ukarabati wa kisima cha uzalishaji wa gesi asilia inaendelea. Ziara hiyo ilifanyika Oktoba 26, 2024.
Post a Comment