Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Maonesho ya wiki ya huduma za fedha
Tanzania Mhe. Adolf Mkenda ambae ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
amesifu shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ya kusimamia
sekta hiyo muhimu kwa taifa huku akiitaka taasisi hiyo kuendelea kuweka
miundombinu itakayovotia wawekezaji wengi zaidi wa sekta ya bima kutoka
Tanzania.
Ameyasema hayo mapema leo wakati alipotembelea Banda la TIRA kwa ajili ya
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Waziri Mkenda
amesema, sekta ya bima mbali ya kusaidia kukinga majanga mbalimbali yanayotokea
lakini pia ni sekta ambayo watanzania wanapaswa kutumia fursa iliyopo ili
kuweza kuwekeza kwa kufungua kampuni ili kuweza kujiingizia kipato binafsi na
taifa kwa ujumla.
Akijibu swali kuhusu njia zinazofanywa na Mamlaka ili kuvutia uwekezaji kwa
wazawa, Mwanasheria Jamal Mwasha ambae ni Msajili wa Migogoro ya Bima katika
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima amesema Sheria ya Bima sura ya 394
kupitia kifungu cha 16 imeweka sharti kuwa kila kampuni inayoanzishwa nchini,
lazima walau theluthi moja imilikiwe na wazawa.
Kwahiyo Mamlaka ina hakikisha kifungu hiki kinazingatiwa ipasavyo na sharti
hilo linatimizwa, amesema pia Mamlaka inatumia majukwaa mbalimbali inapokutana
na wawekezaji na wadau wa sekta nyingine kuwapa elimu juu ya fursa zilizopo na
kumekua na mwitikio mzuri.
Mwasha memalizia kusema kuwa
Mamlaka inasaidia uanzishwaji wa Konsotia ya Bima ya Kilimo ambapo ni
muunganiko wa kampuni wazawa walioweka mtaji ili kuweka ufanisi katika
utekelezaji wa Skimu ya Taifa ya Bima ya Kilimo na kuongeza uwezo wa kimtaji wa
soko la bima nchini kwa ajili ya kukinga majanga kwenye sekta ya kilimo.
Post a Comment