Waziri Mkuu Majaliwa akizungumza katika hafla ya kuaga miili ya waliopoteza maisha kutokana na kuporomoka kwa jengo hilo mapema Jumamosi, inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema amesema watu 16
wamefariki na wengine 86 wameokolewa katika ajali ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo
Waziri Mkuu Majaliwa
amesema hayo katika hafla ya kuaga miili ya waliopoteza maisha kutokana na
kuporomoka kwa jengo hilo mapema Jumamosi, inayofanyika katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema
kwa maelekezo ya serikali inaendelea kugharamia matibabu ya wahanga wote na
hakuna anayetozwa huku waliofariki serikali inagharamia miili yote ya marehemu
mpaka katika nyumba zao za mwisho.
“Mpaka
sasa serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa
mitungi ya gesi kwa watu waliopo chini,kutafuta vitendea kazi kwa ajili ya watu
wanaofanya uokozi”Waziri Mkuu Majaliwa
Aidha
Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imeunda tume ya watu 19 ambayo itafanya
kazi ya kuyapitia majengo yote ya Kariakoo ili kujua ubora wa majengo hayo na
shughuli zinazoendele kwani mahitaji ya soko hilo bado yapo palepale.
Awali
akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) William Lukuvi amesema uchunguzi
wa awali juu ya kuporomoka kwa jengo hilo unaendelea kufanywa huku akisisiza
wadau kutoa michango yao kwenye akaunti maalum.
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema yupo tayari kuwajibika na
kwamba cheo alichonacho siyo mali kuliko uhai wa watu iwapo itabainika kuwa
hakuwajibika kikamilifu katika uokozi wa jengo lililoporomoka Kariakoo.
Naye Mbunge wa Ilala na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania,Mussa Hassan Zungu amesema Taifa limepoteza watu muhimu huku akishukuru namna wananchi wa Ilala walivyojitoa na kusimama na Taifa kukabili tukio hilo
Post a Comment