AAT KUSHIRIKIANA NA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI

...................

Na Magrethy Katengu Dar es salaam

Elimu ya Usalama barabarani  haina hudi kuwa ya  lazima kutolewa kwa wanafunzi  na  ianzie ngazi ya chini yaani shule ya msingi ili kusaidia watoto kuondokana na changamoto ya ajali zinaweza kuwatokea  wanapotoka majumbani kuelekea shuleni au shuleni kurudi nyumbani.

Ameyasema hayo leo Novemba 5, 2024 Jijini Dar es salaam Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wakili mwanasheria wa kikosi cha Usalama Barabarani Deus Sokoni wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Alhasan Mwinyi iliyopo Kinondoni  kutekeleza Mradia wa Assessment project kwa kushirikiana na chama cha mbio za magari ( Automobile Association AAT)ukiwa na  lengo la kutoa elimu ya kuwajengea watoto wa shule za msingi na Sekondari namna ya kuishi kwa usalama wakiwa salama barabarani bila kupata dhara lolote.

" Mradi huu  tumekuwa tukiufanya kwa kushirikiana na wadau wa  Chama cha mbio za magari (Automobile Association Tanzania  AAT )  kwenda nao katika shule mbalimbali na tulianzia  Wilaya ya Temeke  sambamba na Kikosi cha Usalama barabarani kwani kufanya hivi tunareje maelekezo ya Serikali kuwa elimu ya Usalama barabarani ianzie ngazi ya chini kabisa" amesema Marakibu Deus

Hata hivyo amesema wamewapatia elimu itakayowasidia kukua na kufahamu ni kosa kisheria kukubali kupanda bodaboda moja watu zaidi ya wanne kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wamekuwa wakichangishana  fedha ili watoto waende shule alfajiri na wamekuwa wakikamatwa na polisi bodaboda wakijetetea uchumi wa wazazi wao hauruhusu kupanda pikipiki moja wanafunzi wawili  .

Sambamba na hayo Mrakibu amebainisha kuwa licha ya kuwapatia elimu ya Usalamaa barabarani pia wamewapatia elimu ya usalama barabarani namna ya kuepukana  na vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyoweza kutendewa na waendesha magari au pikipiki kwani kuna  watu ambao siyo waaminifu wamekuwa na tamaa wakiwarubuni na kuwatendea vitendo ikiwemo ulawiti, ubakaji, hivyo kuwapelekea wengine kukatiza ndoto zao za kimasomo .

Kwa upande wake Athumani  Kasanga Meneja wa kukuza biashara AAT chama cha mashindano ya magari  amesema  wamekuwa wakienda katika mashule mbalimbali  kuangalia hali ya miundombinu na kujenga  barabara zenye alama(Zebra cross)  kwa kushirikiana na kikosi cha usalama huku  wakitoa mafunzo namna ya kutumia barabara wasipate madhara yeyote wanapoenda shule na kurudi nyumbani

"Sisi kama taasisi inayojihusisha na  michezo ya magari burudani hii  inafundisha watoto kujua nidhamu ya vyombo moto hususani magari na   kuwatoa katika michezo hatarishi " amesema Athumani

Na kwamba pia elimu ya usalama mashuleni na wamefanya ni kwa  mara ya 3 hufanyika  kila mwaka na tayari   meshafikia shule saba kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani.

Aidha pamoja na kuwafikia watoto pia wamefanikiwa  kuwafikia bodaboda zaidi ya  5000 kuwapatia elimu huku wakiwapatia elementi na vifaa vingine vya kufanyia shughuli zao bure kwa









 

0/Post a Comment/Comments