Wakala ya
Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam inatekeleza mradi wa
matengenezo (maintenance) ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu
ya kwanza chini ya mradi wa OPBRC (Output and Performance-Based Road Contract)
uliosainiwa rasmi tarehe 07 Septemba 2018.
Mradi huu
ni wa muda mrefu (Long term contract) ulianza rasmi tarehe 01 Aprili 2019
ukitekelezwa na mkandarasi M/s Bharya Engineering & Contracting Co. Ltd
(BECCO) kwa utekelezaji wa mradi kwa muda wa miezi sitini (60) yaani miaka
mitano (5).
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar
es Salaam Mhandisi John Mkumbo leo tarehe 5 Novemba 2024 na kueleza kuwa mradi
huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 18.509 ambazo zinajumuisha makundi
matatu ya kazi.
Ameyataja
makundi hayo kuwa ni Pamoja na Mradi wa matengenezo ya miundombinu ya mabasi
yaendayo haraka (BRT) awamu ya kwanza yenye urefu wa kilomita 21.4 ikihusisha:
Barabara ya Morogoro kuanzia Ferry mpaka Kimara Mwisho, Barabara ya Kawawa
(Magomeni Mapipa – Morocco); na Barabara ya Msimbazi (Fire – Msimbazi BRT
Station).
Mhandisi
Mkumbo amesema kuwa TANROADS pia inatekeleza kazi za maboresho ya sehemu
zilizoharibika (Rehabilitation works) ikihusisha Matengenezo makubwa ya tabaka la
lami katika sehemu zilizokuwa zimeharibika. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni
Ubungo maji, Kibo, Corner, Baruti, Bucha, Korogwe na Kimara Mwisho. Tabaka la
lami katika maeneo haya liliondolewa (milling) pamoja na kuwekwa lami mpya kwa
kutumia technolojia ya Superpave (SP 12.5), Kuweka nguzo za zege (precast
concrete poles C20/guard posts), Ujenzi wa sehemu za watembea kwa miguu (paving
blocks), Ujenzi wa kingo za barabara (Kerbstones) na Matengenezo kwenye njia za
waendesha baiskeli.
Pia
TANROADS Dar es salaam imefanya kazi za dharula (Emergency works). Kazi hizi
zinahusisha matengenezo ya uharibifu ambao haukutarajiwa (unforeseable events
that are beyond the control). Kazi hizi ni pamoja na; Kuondoa tope, mchanga na
takataka kwenye daraja na eneo la barabara wakati wa mafuriko na mvua kubwa, na
Matengenezo ya miundombinu yatokanayo na ajali za barabarani kwenye miundombinu
ya BRT awamu ya kwanza.
Mhandisi
Mkumbo ameeleza kuwa kazi za matengenezo zimefanyika wakati wote (OPBRC
maintenance works). Kazi hizi zinahusisha; Urudishiaji wa michoro ya barabara
(road marking), Uwekaji wa alama za barabarani (road signs),
Matengenezo/uzibuaji wa mitaro ya maji ya mvua (underground drainage systems)
ndani ya uwanda wa km 21.4 za mradi, Kuweka mifuniko ya zege kwenye mifumo ya
maji (chambers), Kuondoa mchanga kwa kufagia barabara ndani ya Km 21.4 kila
siku.
Kazi
zingine ni Pamoja na Kufyeka majani na kutunza maeneo yenye bustani (green
areas) ndani ya eneo la mradi, Kuondoa vichaka na kupunguza miti (prunning) iliyo
pembezoni mwa barabara (road reserve), Kuziba viraka/mashimo, Matengenezo
madogo ya madaraja yaliyopo ndani ya mradi, Marekebisho ya njia za waenda kwa
miguu/baiskeli, Matengenezo ya nguzo za zege zinazoharibika, Matengenezo ya
maungio ya zege (joint sealing), Marekebisho ya mifuniko (catchpit grating), na
Kuzibua mifereji yote iliyo kwenye eneo la mradi.
MWISHO
Post a Comment