**
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema imebaini kuwepo kwa majukwaa na programu tumizi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila kuwa na leseni au idhini kutoka kwa Benki Kuu.
Kupitia taarifa iliyoitoa BOT, imesema Hali hiyo
inahatarisha usalama wa wateja na ustawi wa sekta ya kifedha, kwani majukwaa
haya yanashindwa kutimiza matakwa ya Mwongozo wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa
Daraja la Pili kwa mwaka 2024.
Mwongozo huu, uliozinduliwa tarehe 27 Agosti 2024, unalenga kuimarisha
usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha nchini na kuhakikisha watekelezaji wa
kanuni zinazolinda wateja.
Hii inajumuisha uwazi katika utoaji wa huduma, uwekaji wa tozo na riba, njia za
ukusanyaji wa madeni, na kulinda faragha ya taarifa binafsi za wateja.
Benki Kuu imefafanua kwamba majukwaa na programu tumizi zinazohusishwa na
utoaji wa mikopo kidijitali ambazo hazijapata kibali kutoka kwa Benki Kuu
haziruhusiwi kuendelea na shughuli hizo.
Post a Comment