CCM YASIKITISHWA NA KIFO CHA KATIBU WAKE WILAYA YA KILOLO IRINGA


......................

Chama cha Mapinduzi, kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu Ya Ccm Taifa, Itikadi, Uenezi Na Mafunzo CPA. Amos Gabriel Makalla imesema kuwa  Marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria Semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha ghafla na cha kikatili.

Amewataka wanachama wa chama hiyo wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.

0/Post a Comment/Comments