CCM YAWEKA WAGOMBEA KWENYE NAFASI ZOTE, UPINZANI 38%


......................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefanikiwa kuweka wagombea katika nafasi zote za vijiji, vitongoji na mitaa huku upinzani ukiweka wagombea 30,977 sawa na asilimia 38 ya nafasi zote 80,430 zinazoshindaniwa.

Waziri Mchengerwa amesema nafasi zitakazogombewa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 ni mwenyekiti wa kijiji nafasi 12,280, mwenyekiti wa mtaa nafasi 4,264 na mwenyekiti wa kitongoji nafasi 63,886, wajumbe wa serikali ya kijiji 230,834 na wajumbe wa kamati ya mtaa 21,320.

Amesema nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama 18 vya siasa viliweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35 ya nafasi hizo na nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni 4,264 ambapo vyama 18 vya siasa viliweweka wagombea katika nafasi 3,281 sawa na asilimia 76.94 ya nafasi hizo.

0/Post a Comment/Comments