CHALAMILA ATOA POLE KWA FAMILIA YA LAWRENCE MAFURU

                  *********

Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamAlbert Chalamila leo Novemba 13, 2024 akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila pamoja na Kamanda wa Kanda Maalumu Afande Jumanne Muliro, amefika na kutoa pole kwa familia ya Bwana Lawrence Mafuru aliyefariki   Dunia Novemba 09, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Apollo Nchini India.

Bunju A, Wilaya ya Kinondoni amemfariji Mke wa Marehemu, Ndugu Jamaa na marafiki kwa kufikwa na msiba huo mzito ambapo amesema " Namna pekee ya kumuenzi Mafuru ni kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa masilahi mapana ya Taifa na watu wake"

Vilevile RC Chalamila amesema yeye binafsi anaendelea kumuombea kwa mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema peponi.






0/Post a Comment/Comments