CHAMA CHA WAAJIRI ATE NA TUCTA WAKAMILISHA MRADI WA KUKUZA UJUZI KWA VIJANA




Kulikuwa na kila sababu ya kusherehekea baada ya kukamilika kwa mafanikio mpango wa kuendeleza ujuzi na stadi za kazi ulioendeshwa na chama cha Waajiri nchini Tanzania(ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) chini ya ufadhili wa mashirika ya viwanda na maendeleo ya Denamark ; Danish Industry(DI) na Danish Trade Development Agency(DTDA) ,katika sherehe za kutamatisha mradi huo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 8 mwaka huu.

Katika tukio hilo la kushereheka kukamilika kwa mradi wa kuendeleza ujuzi, stadi za kazi na kuwapa vijana uwezo wa kuajirika, waendeshaji wa mradi na wahisani waliwasilisha kwa serikali ushauri wa jinsi ya kukuuza na kuendeleza ujuzi na stadi za kazi.

Mpango huu ambao ulizinduliwa rasmi mwaka 2021, umekamilika kwa mafanikio ikiwa ni miaka minne tangu kuanza kutekelezwa nchini.

Hafla hiyo ya kuadhimisha kutamatika kwa mradi ilihudhuriwa na Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Professa Adolf Mkenda ambaye alielezea changamoto nyingi zinazolikumba bara la Afrika kutokana na tatizo la ukosefu wa ajira.



Kwa kuona changemoto hizo, Waziri Mkenda alitilia mkazo uwepo wa mahusiano ya karibu kati ya taasisi kama VETA na waajiri ili waweze kupata njia bora ya kukuuza mitaala itakayo boreshaji pia ujuzi na stadi za kazi na kukuuza soko la ajira kwa vijana.
Katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu(CEO) wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) Suzanne Ndomba – Doran aliwashukuru wadau na wahisani wa mradi huo na kuahidi kuendelea kuunga mkono zoezi zima la kuendeleza na kuberesha ujuzi na stadi za kazi nchini.

Vilevile, Afisa Mtendaji Mkuu alisema ATE itazindua hivi karibuni mabaraza ya kuendeleza ujuzi na stadi za kazi katika kila sekta nchi nzima kwa ajili kuboresha zaidi ujuzi katika maeneo ya kazi na kudhibiti ukosefu wa ajira .

Wakati wa majadiliano ya vikundi husika, wawakilishi kutoka taasisi za kutoa ujuzi kama VETA na Don Bosco, NACTVET, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, waaajiri kama Kampuni ya Sukari Kilombero na TBL, TAeSA, Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu waliiunga mkono kazi iliyofanywa na TUCTA na ATE ambayo ililenga zaidi kwenye uboreshaji wa ujuzi na soko la ajira kwa vijana

Katika hafla hiyo, wadau na wahisani wa mradi walikabidhiwa vyeti kwa mchango wao mkubwa uliowezesha mradi kufanikiwa.





0/Post a Comment/Comments