Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya
Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo wakati
akizungumzia na waandishi wa habari jijiji Dar es salaam kuhusu operesheni ambayo wameifanya kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya dola ambayo imefanyika kuanzia Novemba 13 hadi 20 mwaka huu.
Gari aina ya Scannia lenye namba za usajili wa Afrika Kusini LN87XJGP ambalo limekuwa likitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi
.......................
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata Jumla ya Kg 2,207.56 za Dawa za Kulevya na Dawa tiba zenye asili ya Kulevya katika Mikoa ya Tanga na Dar es salaam.
Pia Mamlaka hiyo imesema inawashikilia watuhumiwa saba wanaohusiana na Dawa hizo ambazo ni pamoja na skanka Kilogram 1,500,Methamphetamine Kg 687.76 ,Heroin Kg 19.2 na Chupa 10 za Dawa tiba zenye asili ya Kulevya aina ya Fentanyl.
Akizungumza jijini Dar es salaam Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo wakati akizungumzia operesheni ambayo wameifanya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ambayo imefanyika kuanzia Novemba 13 hadi 20 mwaka huu.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa Nov 14 mwaka huu jijini Dar es salaam katika Wilaya ya Kigamboni waliwakamata watuhumiwa Mohamed Suleiman Bakari (40) na Sullesh Said (36) wakazi wa mabibo wakiwa na kilogram 1,350 za Dawa za Kulevya Ina ya skanka zikiwa zimefichwa kwenye nyumban ya kupanga.
Kamishna Lyimo amesema kuwa dawa nyingine zilipatikana ndani ya gari aina ya Nissan Juke yenye namba za usajili T 534 EJC zikiwa tayari kusambazwa.
"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 imeweka katazo kwa mmiliki au msimamizi wa nyumba,msimamzi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike kwa lengo la kutengeneza ,kuvuta,kujidunga ,kuuza au kununua dawa za kulevya,"amesema Kamishina Jenerali Lyimo.
Aidha Kamishna lyimo amesema kuwa pia katika mtaa wa Pweza Sinza E Wilaya ya Ubungo Nov 17 mwaka huu katika jiji la Tanga watuhumiwa Ally Kassim Ally mwenye umzi wa miaka 52 na Fadhadi Ally (36) walikamatwa mtaa wa Mwakibila wakiwa na Kilogram 706.96 za dawa aina ya Heroin na Methamphetamine.
Ameendelea kusema kuwa Nov 19 mwaka huu katika mtaa wa Kipata na Nyamwezi Kariakoo jijini Dar es salaam Mamlaka iliwakamata watuhumiwa Michael Dona Mziwanda (28) mkazi wa Tabata Segerea na Tumpale Mwasakila (32) mkazi wa Temeke wakiwa na chupa kumi za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl wakiwa nazo katika duka la Mpesa.
Katika Hatua nyinine Kamishna Lyimo amewatahadharia waganga wa kienyeji ambao wametumika kuwaaminisha watuhumia kujihusisha na usambazi wa dawa hizo kuwa hawatokamatwa kwani serikali ipo macho wakati wote.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imewataka wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyumba zao,kwani inayotumika kwa shughuli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa,na anapojua kosa linatendekea katika nyumba hizo anajukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka
Post a Comment