DKT. MAGESA AONYESHA KURIDHIKA NA UTENDAJI WA MSD KANDA YA MBEYA

*******
Mjumbe wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (MSD), Dkt. Alex Magesa, ameonyesha kuridhika na utendaji kazi wa MSD katika Kanda ya Mbeya baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu.

 Ziara hii ililenga kutathmini hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katika ziara hiyo, Dkt. Magesa alitembelea hospitali ya rufaa ya Mbeya, vituo vya afya vya Chizuvi na Ilambo, pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Songwe.

Akiwa kwenye maeneo hayo, Dkt. Magesa alikiri kupokea mrejesho mzuri kutoka kwa wahudumu wa afya na viongozi wa afya kuhusu upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, ambapo alibaini kuwa asilimia 90% ya mahitaji ya dawa na vifaa vimetimizwa ipasavyo na MSD.

Hata hivyo, Dkt. Magesa alitaja changamoto za miundombinu, hasa ubovu wa barabara zinazounganisha maeneo mengine ya mkoa, hasa Chizuvi, ambazo zinachelewesha usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

 Alikiri kuwa changamoto hii inahitaji kutolewa kipaumbele na aliahidi kufikisha taarifa hizi kwa bodi ya MSD na mamlaka za juu ili kuchukuliwa hatua za haraka.

Ziara hii inadhihirisha juhudi za MSD katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati, licha ya changamoto zinazokabili usambazaji katika baadhi ya maeneo.







 

0/Post a Comment/Comments