DKT. MPANGO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA GCA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI

                    *******

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Duniani (GCA) Prof. Patrick Verkooijen. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.

 Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Taasisi hiyo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Cosato Chumi, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (New York) Mhe. Balozi Hussein katanga pamoja na Mshauri wa Rais kuhusu mabadiliko ya tabianchi Dkt. Richard Muyungi.







0/Post a Comment/Comments