MAHAKAMA YAMUACHIA DKT NAWANDA


........................

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa ikimkabili. 

Katika uamuzi wake kwenye kesi hiyo ya jinai namba 1883/2024, yenye kosa la kulawiti, uliosomwa na Hakimu, Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Erick Marley.

Katika uamuzi huo, Hakimu Marley amesema mahakama hiyo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa Dk Nawanda hatiani na hivyo kumwachia huru.

Muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kumuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda, mwanasiasa huyo ametoa kauli yake kuhusiana na uamuzi huo.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, naishukuru familia yangu, naishukuru mahakama imetenda haki, namshukuru kaka yangu Alex kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, basi Mungu ni mwema, kila kitu kinatoka kwa Mungu, utukufu unatoka kwa Mungu,” amesema Dk Nawanda.


0/Post a Comment/Comments