....................
Na Magrethy Katengu-
Dar es salaam
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Kamanda DCP Ramadhani Ng'azi amesema suala la elimu ya usalama barabarani ni muhimu na linalohitaji kuunganisha nguvu za pamoja ili kuokoa kundi hilo kwa bahati mbaya wao ni miongoni mwa watumia na wako hatarini zaidi wanapovuka barabra za maeneo ya shulea na majumbani .
Akizungumza na wanafunzi na walimu katika shule saba za Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Novemba 7,2024 wakati akifunga mafunzo ya Tathmini za shule zilizopatiwa elimu hiyo Mkuu wa kikosi cha Kamanda DCP Ramadhani Ng'anzi ambapo amesema mafunzo hayo waliyopatiwa baadhi ya waalimu na wanafunzi yanakwenda kuwa chachu kubwa kwa wengine kupunguza ajali za barabarani husasani kwa watoto.
"Kuwapatia waalimu mafunzo hayo ni jambo muhimu kubwa sana kwani mwaalimu mmoja anakutana na darasa moja lenye wanafunzi zaidi ya mia hivyo nawataka mtekeleze kusambaza elimu hii kwa wanafunzi na jamii inayowazunguka ili kusaidia kupunguza ajali zisizo za lazima" amesema Kamanda Ng'azi
Hata hivyo amewasisitiza kuwa wanajukumu kubwa kuyaendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi ili kuhakikisha watoto hao wanakua salama na wanaweza kujilinda wanapokwenda shule au wanaporudi majumbani.
Kamanda Ng'azi amesema Kikosi cha Usalama barabarani wameamua kushirikiana na wadau Chama cha mashindano ya magari (Automobile Association Tanzani AAT ) ili kusaidia. kupunguza ajali za barabarani kwa kutoa elimu kujenga ( Zebra cross) kwa wametambua kuwa zinazotokana watoto ndio nguvu kazi ya kesho na hawana kuwekeza .
Kwa upande wake, Rais wa Chama Cha mbio za Magari Tanzania (AAT) Nizar Jivani amesema kuwa, hali ya usalama barabarani Tanzania, Takwimu inaonyesha kwani kuanzia Januari hadi Septemba 2023 kuliwa na ajali 1,324 zilizorekodiwa ambapo 834 kati ya hizo zilisababisha vifo ikilinganishwa na mwaka 2024 hadi Septemba ajali zimeongezeka na kufikia 1364, ongezeko la asilimia 3.
"Hata hivyo vifo vimeongezeka hadi 920 ongezeko la asilimia 10.3 ya vifo vilivyotokea barabarani, hivyo ni vyema serikali ikaangalie namna bora ya kupunguza ajali za pikipiki ambazo maafa kwa mwaka 2023 kulikua na ajali 481 za pikipiki ambapo zimesababisha vifo 284 mwaka 2024 hadi Septemba ajali za pikipiki zimeongezeka na kufikia 498 na idadi ya vifo imeongezeka hadi 317 ongezeko la asilimia 11.6"
Sambamba hayo amesema , kupitia mradi kutekeleza wa school.Assessment project wamefanya Tathmini za shule walizozipatia elimu ya kwa kuwahoji baadhi ya wanafunzi na kujionea kuwa wameelewa hivyo wanakwenda kusambaza kwa wengine
Naye, Mkurugenzi mtendaji wa AAT Najma Rashid amesema kuwa, katika mzunguko wa kwanza wa mradi huo walizofikia shule 11 katika Wilaya ya Ilala ambapo wamefanya maboresho kw kujenga miundombinu ya shule ikiwemo vivuko na kuweka alama Zebra cross.
" Mradi huu ni awamu ya pili tumezifikia shule 7 katika Manispaa ya Kinondoni ikiwemo Shule ya Sekondari kijitonyama, Magomeni, Turiani, shule ya msingi Tandale Magharibi, Mwalimu Nyerere, Turiani pamoja na Ali Hassan Mwinyi English Medium Pre and Primary.
Naye Janeth Mabusi ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Turiani ameshukuru sana kupatiwa mafunzo hayo ambayo yatakwenda kuwasaidia na kuwajenga wanafunzi kujilinda wanapokua barabarani kwa kufuata sheria zote, huku akiahidi kwenda kuisambaza kwa jamii inayowazunguka watoto wao.
"AAT imewajengea ujasiri watoto wao kwani wamepata mafunzo ya kutosha na wamejifundisha namna bora ya kuwa salama hasa wanapokua barabarani, hivyo tunaomba na wadau wengine imeitaka kuongeza wigo kwa kuzifikia shule nyingi zaidi ili nao elimu hiyo iwafikie watoto wengi" amesema Mwalimu
Mradi huu umefadhiliwa na Shirikisho la kimataifa la Magari (FIA) unaonesha dhamira ya kutengeneza barabara salama hasa katika maeneo ya shule na kuimarisha mazingira ambapo watoto wanakuw salama wanapokua wakienda shule na kurudi kila siku,
Post a Comment