*********
Mwandishi
wetu Dar es salaam
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii yapongeza
Viwanda vya Elsewedy Electricity na Knauf kwa Utekelezaji wa Sheria za Usalama
na Afya Mahali pa Kazi
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii
imeeleza kuridhishwa kwake na hali ya usalama na afya mahali pa kazi katika kiwanda
cha kutengeneza Nyaya za umeme na Transfoma cha Elsewedy Electric Kigamboni
Jijini Dar es salaam na Kiwanda cha kutengeza gypsum cha Knauf Mkuranga Mkoani
Pwani. Pongezi hizo zimetolewa baada ya ziara ya kamati hiyo katika ofisi za
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na viwanda hivyo, iliyofanyika
Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam na Pwani.
Ziara hiyo iliongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, pamoja na
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda. Wajumbe wa kamati hiyo walitembelea
maeneo ya kazi na kujionea utekelezaji wa sheria za usalama na afya mahali pa
kazi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq, alitoa pongezi
mara baada ya kutembelea viwanda hivyo, amesema Viwanda hivyo vimekuwa mfano
mzuri kwa kufuata sheria na kanuni za usalama na afya mahali pa kazi, akisema
kamati hiyo itaendelea kutoa ushauri kwa serikali kuhusu umuhimu wa kulinda
nguvu kazi ya wafanyakazi
“Tuko na wenzetu wa OSHA ambao ni miongoni mwa taasisi ambazo
zipo chini ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Ustawi na Maendeleo ya jamii ambapo tumetembelea maeneo mbalimbali kuangalia utekelezaji wa sheria ya
usalama na afya mahali pa kazi
Kwa taarifa tulizopata awali Knauf ni miongoni
mwa kampuni ambazo zinafuata sheria na kanuni za usalama na afya mahali pa kazi
vizuri na tumekuja kujionea wenyewe, Sisi
kama kamati tumekuwa tukiishauri
serikali jinsi gani suala la usalama na afya mahali pa kazi linatakiwa liwe ili
kulinda ustawi wa wafanyakazi pindi wanapo kuwa kazini na tutaendelea kuishauri
”alisema Mhe. Toufiq.
Awali akizungumza mara baada ya ziara hiyo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani
Kikwete, alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao ambao
wanazalisha na kusafirisha bidhaa nje ya nchi, hali inayo changia kukuza uchumi
wa Taifa Pamoja na kutoa fursa kwa vijana kupata ajira katika viwanda hivyo.
Sambamba na hayo, Mhe. Ridhiwani aliupongeza Wakala wa
Usalama na Afya Mahali Pa Kazi kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara amabazo zimepelekea viwanda hivyo kuzingatia
masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.
“Nitumie nafasi hii kuupongeza uongozi wa OSHA chini ya
Mtendaji Mkuu Bi. Khadija Mwenda kwenye viwanda vyote tulipo fika kabla ya
kuanza kutembelea kiwanda lazima muingie kwenye chumba maalumu kupata maelekezo ya usalama na afya hususani
kuhusu mambo mtakayo kutana nayo lakini pia namna ya kuweza kujilinda “ alisema
Mhe Ridhiwan
Amesema amefurahishwa namna ambavyo mifumo iliyowekwa Viwandani
hapo vinavyofanya kazi na jinsi vinavyoweza kumlinda mfanyakazi
“Nilicho kipenda zaidi ni namna ambavyo mifumo inavyofanya
kazi Viwandani hapo ukisogelea au kugusa uzio wa mashine, mitambo inazimika yenyewe jambo ambalo ni hatua kubwa
sana katika kulinda usalama wa wafanya kazi, na haya yote ni matokeo ya kaguzi
zinazo fanywa na OSHA mara kwa mara imepekea kufikia hatua nzuri za kiusalama maeneo hayo hali hii ni ishara nzuri ya kazi bora inayo fanywa
na wenzetu wa OSHA pia ni ishara nzuri kwa Mtendaji mkuu kuendelea kusimamia
maagizo ya mheshimiwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, sisi wasaidizi wa mheshimiwa
Rais kazi yetu nikuleta ujumbe na kuhakikisha watanzania wanakua salama kama anavyotaka Rais, Kwa hakika naridhishwa sana na kazi
ambayo OSHA mnaifanya “alisema Mhe. Ridhiwani.
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya
Mahali pa Kazi Bi.Khadija Mwenda,
amewasisitiza Waajiri nchini kuendelea kuzingatia sheria ya Usalama na Afya
Mahali pa Kazi.
Bi.Mwenda, amesema maeneo ya kazi yanapozingatia usalama na
afya kunaongeza uzalishaji kutokana na kupunguza vihatarishi kwenye maeneo yao
na hivyo kuongeza uzalishaji.
“leo tulikuwa na Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendelo ya
Jamii ambayo ilikuja kuangalia jinsi ambavyo OSHA inasimamia sheria ya usalama
na afya mahali pa kazi, kimsingi huu ni utekelezaji wa maelekezo tuliyo pewa tulipo kutana na Kamati ya Bunge
tulitoa taarifa nzuri na kamati
wakaridhishwa nayo lakini wakataka kujionea na leo wamekuja wamejionea.
kwenye kiwanda hiki cha Knauf uwekezaji unaongezeka mara dufu
kwa sababu ya mazingira na mifumo mizuri iliyopo hivyo nitoe rai kwa wawekezaji
na wafanya biashara wawekeze kwenye mifumo ya usalama na afya ili kulinda
wafanya kazi.” alisema Bi.Khadija Mwenda.
Naye mwanasheria wa kiwanda cha Knauf, Flora Erasto aliishukuru kamati ya
Bunge Pamoja na OSHA kwa kufanya ziara kiwandani hapo huku akieleza kuwa
kiwanda hicho kimekuwa kikifanya kazi kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na OSHA tangu kuanzishwa kwake nah ii ndio
imetufanya kuwa bora zaidi.
“kwanza tunaishukuru sana OSHA tangu
kuanza kwa kiwanda hiki tumekuwa tukifanya kazi na OSHA vizuri na wamekuwa wakitushauri na kutupa
maelekezo muhimu kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi , pia
tunaishukuru serikali kwa kutoa miongozo mizuri na nafasi nzuri ambayo imekuwa
ikitusaidia sisi kama wawekezaji.”alisema Frola.
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa
Kazi ni taasisi iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu wenye jukumu la kusimamia masuala ya usalama na Afya mahali pa
Kazi.
………………………………………………….Mwisho……………………………….
Post a Comment