Utafiti wa hivi karibuni wa jarida la The Lancet unaonyesha kuwa idadi ya watu wazima wanaougua kisukari duniani kote imeongezeka maradufu katika miongo mitatu iliyopita, huku ongezeko kubwa ni katika nchi zinazoendelea.
Utafiti unabainisha kwamba tatizo la kisukari limeathiri karibu
asilimia 14 ya watu wazima duniani kote kufikia mwaka 2022, ikilinganishwa na
asilimia saba mwaka wa 1990 ambapo Zaidi ya watu milioni 800 duniani sasa
wanaugua kisukari.
Watafiti wamesisitiza kuwa unene kupita kiasi ni sababu kubwa
inayochangia kisukari aina ya 2 huku pengo la kutibu ugonjwa huo baina ya nchi
tajiri na maskini pia likiongezeka.
Mwandishi
mkuu wa utafiti huo Majid Ezzati wa Chuo cha Imperial London alisema kuwa
kukosekana kwa matibabu thabiti kunahatarisha matatizo mengine ya kiafya kwa
watu wenye umri mdogo haswa katika nchi zenye kipato cha chini.
Cc Dwkiswahili
Post a Comment