Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la nane la uwezeshaji wananchi kiuchumi linalotarajiwa kufanyika Disemba 3 na 4 mwaka huu mkoani Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
kuhusiana na kongamano hilo Katibu wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi
kiuchumi Beng'i Issa amesema kongamano hilo linatarajiwa kukutanisha wadau
takribani 700 kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali zinazotolewa na taasisi za
serikali
Kadhalika amesema kongamano hilo lililobebwa na Kauli mbiu
isemayo “Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni msingi wa maendeleo ya watanzania”
litatoa fursa ya kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ili
kuweza kubadilishana ujuzi na kupeana fursa za kiuchumi.
Post a Comment