MAMLAKA
ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa kadi 174 za usajili kwa wahudumu wa
mabasi ya abiria ya masafa marefu, ambao wamekidhi vigezo na kusajiliwa.
Akizungumza katika hafla
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David
Kihenzile, alisema utoaji wa kadi hizo kwa wahudumu ni ishara ya kiu ya LATRA
ya kuboresha huduma za usafirishaji nchini.
"Hafla hii ina tafsiri ya ndoto
ya Serikali ya awamu ya sita ya kuboresha maslahi ya watoa huduma, pamoja na
kuboresha sekta mzima ya uchukuzi. Pia, inaakisi mpango kabambe wa kukabiliana
na ajali za barabarani," alisema Naibu Waziri Kihenzile.
Aliongeza kuwa hatua hii ya ugawaji
kadi ni sehemu ya juhudi za Serikali kuongeza ajira na kutoa heshima kwa wahudumu,
ili waweze kutambulika rasmi na kufanya kazi kwa ufanisi.
Aliipongeza Bodi na Menejimenti ya
LATRA kwa kuhakikisha kuwa suala la ubora wa huduma za usafiri linapewa
kipaumbele na uzito, na kusimamia upitishwaji wa wadau katika sekta hiyo.
Kwa upande mwingine, Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Johansen Kahatano, alisema kuwa hatua ya kutoa kadi
za usajili ilianza kwa kuandaa mwongozo wa mafunzo, ambapo Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) na Chuo cha Usafirishaji (NIT) walikuwa waandaaji wa mtaala wa
mafunzo.
Mwenyekiti wa Bodi ya LATRA, Ahmed
Mohamed Ame, alisema hadi kufikia Oktoba mwaka huu, zaidi ya wahudumu 700
walipata mafunzo, na 174 kati yao ndio walikidhi vigezo na kusajiliwa.
"LATRA inatekeleza majukumu yake
kwa mujibu wa kifungu cha (5) (1) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
Ardhini, Sura ya 413, ambapo miongoni mwa majukumu hayo ni
Mmoja wa wahudumu waliopewa kadi
hizo, Gift Manege, aliipongeza LATRA kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatasaidia
kuboresha utendaji kazi wao.
Aidha, aliwaomba wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuwapatia mikataba ya kazi wahudumu, ili waweze kujikwamua kimaisha.
Mwisho
Post a Comment