MSD YATEMBELEA KITUO CHA AFYA ILEMBO, MBEYA VIJIJINI

Ujumbe kutoka MSD umefika Kituo cha Afya Ilembo kilichopo wilaya ya Mbeya Vijijini. Kituo cha Afya Ilembo ni mnufaika wa mradi wa CEmONC na kinahudumiwa na Kanda ya Mbeya.

Ujumbe huo, ukiongozwa na mjumbe wa Bodi, Dr. Alex Magesa, ulipata fursa ya kujionea huduma zinazotolewa katika kituo hicho na kuwakumbusha watumishi kuendelea kutoa ushirikiano kwa MSD ili kufanikisha ukamilishwaji wa mnyororo wa ugavi na upatikanaji wa huduma bora za afya.

MSD inasherekea kutimiza miaka 30 ya kuokoa maisha na kusimamia kikamilifu majukumu yake ya uzalishaji, ununuzi, utunzaji, na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

Naye kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ilembo, Dkt. Apolinali Lucas Chove, ameipongeza MSD kwa kuwa mhimili mkubwa katika sekta ya afya, akisema kwamba huduma za dawa na vifaa tiba zinawafikia wakazi kwa asilimia 80%, hivyo kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa wakati.






0/Post a Comment/Comments