Kushoto Mr. Alfa Chiwanga Manager mkuu wa Mahesabu (Finance Manager) akiwa na Regina Maduka Manager Rasilimali Watu( kulia) wakikabidhi msaada wa mahitaji muhimu kwenye zoezi la Uokoaji linaloendelea Kariakoo.
*****
Uongozi wa OYA Microcredit Watoa Msaada kwa Waathirika wa Ajali Kariakoo
Uongozi wa Kampuni ya ukopeshaji mikopo ya OYA Microcredit na wafanyakazi wake wametoa mchango wa mahitaji muhimu kwenye zoezi la uokoaji linaloendelea Kariakoo.
Akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio kutoa msaada huo, Meneja Rasilimali Watu wa OYA, Regina Maduka, amesema wanatoa msaada huo kwa wote waliopoteza wapendwa wao na wataendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha msaada unafika pale unapohitajika.
Aidha, amesema kuwa Watanzania wote ni ndugu na kwa pamoja wanaweza kutengeneza Tanzania bora zaidi.
‘‘Siku ya leo tumesimama pamoja na jamii nzima ya Tanzania hasa walioathirika na ajali hii, tukidumisha utamaduni wetu wa ushikamano na upendo katika kukabiliana na changamoto kama hizi,’’ amesema Maduka.
Post a Comment