Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni akizungumza leo katika uzinduzi wa mpango mkakati wa ujanibishaji ambao umefanyika katika hotel ya Hyat iliyopo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa miradi ya Save The Children Tanzania Anatory Rugaimukamu akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa ujanibishaji ambao umefanyika katika hotel ya Hyat iliyopo jijini Dar es salaam.
Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi na Haki za Binadamu (THRDC) Onesmo Olengurumwa (katikati) akishiriki katika uzinduzi wa mpango mkakati wa ujanibishaji ambao umefanyika katika hotel ya Hyat iliyopo jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki walioshiriki katika uzinduzi wa mpango mkakati wa ujanibishaji ambao umefanyika katika hotel ya Hyat iliyopo jijini Dar es salaam.
..............................
NA MUSSA KHALID
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Save the Children limesema litaendelea kuwajengea uwezo washirika wa maendeleo kuhakikisha juhudi zinamfikia kila mtoto na kumjengea mazingira salama katika kiafya,kielimu,ulinzi na katika haki zake kama mtoto.
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mpango mkakati wa ujanibishaji ambao unalenga kufanya juhudi za maendeleo ziwe na ushawishi kwa wale waliokaribu na mahitaji ya jamii husika ambao umewashirikisha wadau na taasisi mbalimbali nchini.
Akizungumza katika Halfa hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni amesema kuwa malengo yao ni kujaribu kubadilisha mitazamo kwa kuruhusu kufanya kazi na mashirika mingine kwa kuwajengea uwezo ili waweze kuwafikia watoto kwa dhamira njema.
Amesema kumekuwa na mapinduzi makubwa ya kuweka mabaraza ya watoto na yakasimama pia wametengeza sera kwa ajili ya kutokomeza ndoa za utoto ambapo wameamua kushirikiana ili kuleta uchechemuzi katika kuwasaidia watoto.
‘Pia Save The Children tunawajengea uwezo watoto wajisemee katika mapambano dhidi ya ukatili katika familia zao na ndio maana tukaamua kutengeneza Baraza la watoto ili kuweza kutushauri kuhusu miradi itakayoleta mabadiliko Tanzania’amesema Kauleni
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamizi wa miradi ya Save The Children Tanzania Anatory Rugaimukamu amesema kila mtu anawajibu wa kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa watoto ili kuepukana na matukio ya ukatili yanayowakabili.
Amesema kuwa wadau wao wanaofanya nazo kazi ni vyema wakahakikisha juhudi za kimaendeleo zinaweza kumfikia kila mtototo sambamba na kuwajengea mazingira salama katika kuwalinda.
Sofia Leghela ni Mratibu wa Jukwaa la Haki za Watoto Zanzibar (ZCRF) amesema wameshirikiana na Shirika la Save the Children katika kuimarisha haki za watoto ambapo wamefanikiwa mpaka sasa kwa upande wa Zanzibar kuhakikisha watoto wanapata nafasi ya kuingia kwenye bajeti ya serikali lakini pia wamekuwa na muongozo mpya wa baraza la watoto kwa Zanzibar kwenye mradi huo.
Sofia ametumia fursa hiyo kueleza kuwa bado kunachangamoto ya vitendo vya ukatili na udhalilidhaji dhidi y awatoto hivyo kupitia mradi huo wanawajengea pia uwezo watoto kulinda na kuzitetea haki zao.
Naye Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi na Haki za Binadamu (THRDC)
Onesmo Olengurumwa amelipongeza Shirika la Save the Children kwa kuongeza ushirikiano na asasi za kiraia nchini katika kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto.
Olengurumwa amesema wanapojengewa uwezo kwa asasi za kiraia za ndani kunakuwa na uhakika wa kujipatia maarifa na uhuru wa kufanya na kufuatilia mambo mbalimbali yanayowakabili watoto.
‘Serikali ione kwamba kuna umuhimu wa kuboresha sera na sheria za nchi ili iweze kuongoza vizuri utaratibu wa kufanya ujanibishaji wa miradi inayotoka nje kwa ajili ya kuboreha utendaji na uwezo sambamba na kuongeza ukuaji wa sekta za asasi za kiraia Tanzania’amesema Olengurumwa
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu Save the Childen ametumia fursa hiyo kuyasisitiza na kuyakaribisha mashirika la Kitanzania kwaamini katika ufanyaji wa miradi ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto hata mmoja anabaki nyuma.
Post a Comment