**********
Serikali imeshauriwa kuzingatia na kuimarisha mazingira wezeshi ya sera na kodi ili kukuza mapato ya serikali na kuendeleza ukuaji wa biashara nchini.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti Breweries Ltd (SBL), John Manyanja, wakati wa ziara ya Kamati ya
Bunge ya Wizara ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Uvuvi katika kiwanda chao kilichopo
Chang'ombe jijini Dar es Salaam .
Manyanja amesema kuwa punguzo la ushuru linaacha pengo la
ushuru wa asilimia 32 ikilinganishwa na bia inayotengenezwa kutoka shayiri
inayooagizwa kutoka nje, ambayo inatozwa ushuru wa shilingi 918 kwa lita.
Watengenezaji wa bia wanaoagiza kutoka nje wanakabiliwa na gharama za ziada za
kulipia ushuru wa uagizaji na athari za mabadiliko ya thamani ya fedha za
kigeni.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deo Mwanyika, amesema kuwa wamesikiliza
changamoto, hasa za kikodi, na watakikisha wanafikishia serikali ili
kutatuliwa.
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe,
amesema kuwa serikali itahakikisha inatengeneza mazingira wezeshi ili kusaidia
wawekezaji wa viwanda na biashara kufanya kazi kwa ufanisi.
Kamati hiyo inatarajia kukutana na wadau tena kutoa muongozo ili kuhakikisha mazingira yanayofaa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya ndani, ambayo yatawezesha mabadiliko ya kiuchumi ya Tanzania na kusaidia kujenga uchumi wa kujitegemea na wenye ustahimilivu.
Post a Comment