SERIKALI YATAKA CHUO CHA KODI KUFANYA TAFITI ZA FORODHA NA KODI




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.

********
Na Mwandishi Wetu 

Serikali kupitia wizara ya Fedha imekitaka chuo cha kodi (ITA) kufanya tafiti ambazo zitatatua changamoto katika mfumo wa forodha na kodi nchini na kujenga mfumo bora wa kodi ambao utarahisisha ulipaji wa kodi kwa hiyari.

Hayo ameyasema jana jijini dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akimwakilisha Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kwenye Mahafali ya kumi na saba kwenye chuo cha kodi (ITA) ambapo wamehitimu jumla ya wahitimu 417.

Elijah amesema Chuo kijikite na tafitia ambazo zitatoa suluhu za changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi huku mapendekezo mengi kwenye tafiti yanakosa utafiti kwenye jamii hivyo yataleta mapendekezo na tafiti kwenye kufikia malengo wanayoyataka.

Aidha Elijah Amewasisitiza Chuo kiendelee kutoa mafunzo ya viwango vya juu kuzingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani ndipo dunia inapoelekea kwa sasa.


Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Kodi Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema baraza lililopo liendelee kufanya kazi ili kufanikisha watumishi ambapo itawezesha kuongeza idadi ya walipa kodi pamoja na kuongeza ulipaji kodi kwa nchi na wataendelea kuboresha miundombinu ili watoe wahitimu bora kwa maendeleo ya nchi.

"Dhamira ya Chuo cha Kodi ni kukifanya kuwa cha kimataifa chenye kutoa wahitimu wabobezi katika masuala ya Forodha na Kodi" amesema Mwenda. 

Naye, Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Isaya Jairo amesema Chuo kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha na kodi  kwenye misingi ya kujenga umahiri na kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kutumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi na itasaidia wahitimu hao waendane na kasi ya teknolojia na forodha ya dunia ya sasa.

 Amesema pia kimekuwa kikitumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi kwa  sasa ambayo itawasaidia wahitimu hao kuendana na  dunia ya sasa

 Chuo hicho kimetunuku vyeti kwa wahitimu 417 wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024 huku idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 wametunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF),Wahitimu 28 wametunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM),

61 wametunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 wametunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akiwakabidhi zawadi wahitimu waliofanya vizuri katika masomo.









Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.

Mkuu wa Chuo cha Chuo Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.

0/Post a Comment/Comments