Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam
imesema jitihada zinazofanyika za kuielimisha jamii kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa
kuelekea uchaguzi ni kutimiza katiba ya Tanzania ibara ya 21inayozungumzia haki
ya kuchagua na kuchaguliwa na mwananchi kushiriki zoezi hilo.
Mkuu
wa TAKUKURU Wilaya ya Kigamboni Emmanuel Boayi Tarmo amesema hayo wakati alipowapa
semina elekezi wadau wa usafirishaji wa bajaji kuhusu kwenda kusimamia na kutoa
elimu kupitia vyombo vyao yenye ujumbe muhimu wa "Tumia vyema fursa ya kuchagua au kuchaguliwa bila vitendo
vya Rushwa"
Tarmo amewapongeza maafisa wa usafirishaji kwa kuamua kushirikiana na
TAKUKURU kufikisha ujumbe wa Mapambano dhidi ya Rushwa kwa wananchi katika
kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Nov 27 mwaka
huu.
Amesema kuwa kama
TAKUKURU Wilaya ya Kigamboni wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanazuia vitendo
vya Rushwa katika uchaguzi huo kwa kuielimisha umma namna ya kuepukana na
vitendo hivyo.
‘Hawa wenzetu
wasafirishaji tumekuwa tukishirikiana kwa muda mrefu katika mapambano dhidi ya
Rushwana wao kwa hiyari hao wamejitolea kama wananchi wazalendo wa Tanzania
kubeba ujumbe wa kuzuia vitendo vya Rushwa katika uchaguzi hivyo niwapongeze
sana kwa julitoa kwao na wametimiza wajibu wao’amesema Mkuu TAKUKURU (W)
Kigamboni
Aidha amewapongeza kwa
kujitoa kwao kwani wametimiza wajibu wakienda sambamba na kauli mbiu ya
TAKUKURU isemayo "Kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu
wetu" jambo ambalo linaimarisha ushirikiano.
Patrick Christopha Kayanda ni Mwenyekiti wa waendesha Bajaji na Pikipiki Wilaya ya Kigamboni –CMPD amesema watahakikisha wanakwenda kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopatiwa na TAKUKURU ili kuifanya Kigamboni kuwa salama katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Hata hivyo Taasisi
hiyo imeendelea kuwasisitiza wananchi kushirikishi mapambano dhidi ya rushwa
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili kweza
kuchagua na kumpata kiongozi aliyebora.
Post a Comment