TAKUKURU YAUNGANA NA WASAFIRISHAJI KUTOA ELIMU YA KUPAMBANA NA RUSHWA

 

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke Ismail Bukuku akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kuhusu ujumbe wanaoutoa kwa jamii kupitia maafisa wa usafirishaji wa bajaji katika Mkoa huo.Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke Ismail Bukuku (kulia) akiwa na viongozi wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikikipi Mkoa wa Dar es salaam (CMPD) Ngazi ya Wilaya ya Temeke wakati akiweka stika maalum katika chombo cha usafirishaji aina ya bajaji yenmye lengo la kutoa ujumbe wa mapambano ya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Nov 27 mwaka huu.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke Ismail Bukuku akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa TAKUKURU mkoa huo sambamba na wadau wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikikipi Mkoa wa Dar es salaam (CMPD) katika eneo la Ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Temeke

Baadhi ya bajaji ambazo zimewekea stika maalum zenye ujumbe wa ‘Tumia vyema fursa ya kuchagua au kuchaguliwa bila vitendo vya Rushwa’

......................

NA MUSSA KHALID

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke kwa kushirikiana na maafisa wa usafirishaji wametoa ujumbe kwa wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Nov 27 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa halfa ya kuwakabidhi maafisa usafirishaji wa bajaji ujumbe muhimu kuelekea wakati wa uchaguzi,Naibu Mkuu wa TAKUKURU (M) Temeke Ismail Bukuku amesema maafisa hao ni wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya Rushwa kwani watakwenda kusambaza ujumbe huo wa uzuiaji wa Rushwa katika Chaguzi za kisiasa.

Aidha Bukuku ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kutumia fursa njema ya kwenda kuchagua viongozi wa serikali za mitaa au kuchaguliwa  bila kutumia Rushwa.

“Tunayo furaha kubwa sisi pamoja na maafisa usafirishaji hapa Temeke kuwahabarisha wananchi juu ya ujumbe wetu unaotoa elimu ya uzuiaji Rushwa katika chaguzi za kisiasa hususani unaofanyika tar 27/11/2024”amesema Bukuku

Amesema kuwa wamejitahidi kutoa elimu ya uzuiaji Rushwa katika chaguzi za kisiasa hivyo wameamua kushirikiana na Maafisa usafirishaji ili kuendelea kusambaza elimu ya mapambano dhidhi ya Rushwa.

‘Tutaweka ujumbe katika bajaji zao ambazo zinasema mwananchi tumia fursa vyema ya kuchagua au kuchaguliwa bila ya vitendo vya Rushwa lakini pia tunasema Mwananchi kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu tukatimize wajibu wetu”ameendelea kusisitiza Bukuku

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikikipi Mkoa wa Dar es salaam (CMPD) Ngazi ya Wilaya ya Temeke Judica Palangyo ameahidi kuwa watahakikisha wanaendelea kufanya kazi viruzi kwa ushirikiano na ikiwa ni pamoja na kusambaza elimu namna ya kuzuia na kupamba na Rushwa Hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ameipongeza na kuishukuru TAKUKURU (M) Temeke kwa kuwaona wasafirishaji kuwa ni sehemu mapambano dhidi ya Rushwa.

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Nov 27 mwaka huu ambapo kwa sasa zinafanyika kampeni za kisiasa kwa kila chama kupitia wagombea wao wananadi sera kwa wananchi.

0/Post a Comment/Comments