*******
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema nchi za Tanzania
na Uganda zitaendelea kushirikiana katika uendelezaji wa miradi mbalimbali ya
Nishati ikiwemo Sekta ya Mafuta na Gesi.
Dkt. Mataragio ameyasema hayo Novemba 22, 2024 jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kushiriki Jukwaa la Kibiashara kati
ya Tanzania na Uganda .
"Tunaangalia ni kwa jinsi gani sekta hii ya Mafuta na
Gesi inaweza ikachangia katika maendeleo ya Nchi hizi mbili, tumekuwa na mijadala
mbalimbali inayolenga kuiendeleza sekta hii ya mafuta na gesi." Amesema
Dkt. Mataragio
Ameongeza kuwa, mjadala
mkubwa katika Jukwaa hilo ni kuangalia namna gani Nchi za Tanzania na
Uganda zinaweza kushirikiana katika sekta za mafuta na gesi.
Mataragio amesema Tanzania na Uganda zinahistoria ndefu
ndefu za mashirikiano akitolea mfano mradi wa kimkakati wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi wa EACOP.
Akiuelezea mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi
(EACOP), Dkt. Mataragio amesema umefikia asilimia 47
Amesisitiza kuwa mradi huo kwa sasa upo katika hatua ya
kutandaza mabomba ambapo takribani kilomita 52 za mabomba zimesha chomelewa ambazo
zitaanza kufukiwa ardhini.
Akizungumzia faida ya mradi kwa wananchi amesema watanzania
wameweza kujengewa uwezo (Capacity building) katika maeneo mbalimbali na hivi
sasa wanafanya kazi kwenye mradi huo.
Kwa upande wa ajira amesema mradi umeweza kutoa zaidi ya
ajira 8000 huku lengo likiwa ajira 10,000.
Post a Comment