Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) limewasisitiza watumiaji wa bidhaa mbalimbali nchini wazisome
taarifa zake kabla ya kununua ikiwemo kuangalia mwisho wa matumizi ili
kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza baada ya kuzitumia.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Afisa Udhibiti Mkuu wa ubora,kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mosses Mbambe wakati
akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia umuhimu wa uwekaji taarifa kwenye
bidhaa na umuhimu kwa watumiaji kusoma taarifa zilizopo kwenye vifungashio
kabla ya kuzitumia.
Mbambe amesema kuwa
suala la uwekaji taarifa kwenye bidhaa lipo kwa mujibu wa sheria lakini pia linaongozwa
na viwango vya bidhaa husika hivyo amewasisitiza wazalishaji kuweka taarifa
hizo kwani zinasaidia mawasiliano baina ya mzalishaji na watumiaji.
Aidha Afisa Udhibiti
huyo amesema kuwa ni vyema watumiaji wakasoma kwa umakini tahadhari ambazo
zinatolewa na wazalishji wa bidhaa ili kuepuka madhara ya kiafya yakiwemo ya
alegi ambayo yanaweza kuwapata.
“Kwa bidhaa ambazo zimewekewa muda wa kuisha kwa
matumizi mfano expire date tumezoea pia kuona use by date na best before hizi
ni lugha ambazo zinatumiwa kwenye bidhaa mbalimbali na ukikuta bidhaa imeandikwa
expire date hiyo inapaswa kuondolewa kwenye soko ukikutana nazo kwenye soko ni
vyema mtumiaji ukatoa taarifa mapema ili Shirika liweze kudhibiti’amesema
Mbambe
Hata hivyo TBS imewataka watanzania kutoa taarifa pindi wanapokutana na bidhaa ambazo zimekwisha muda wake kwenye soko ili Shirika lifuatilie na kuweza kufanya udhibiti kwa wakati.
Post a Comment